Newz: Nay kumjia juu young killer

Baada ya Nay wa Mitego kuachia wimbo wake mpya ‘Moto’ambao ndani yake amewachana wasanii mbalimbali akiwemo rapa Young Killer Msodoki na baadaye Young Killer kuamua kumjibu kupitia wimbo ‘True Boya’, Nay amerudi kivingine tena  
Rapa huyo ambaye ana tabia ya kuachia nyimbo za kuwachana wasanii wenzake, amepost video ya wimbo wake huo kupitia mtandao wa Instagram nakutuma maneno ambayo yanadaiwa kwenda kwa rapa huyo kutoka Mwanza.

“Thanks @cloudsfmtz Muziki Sio kuandika tu Mistari, Nidhamu itakufanya Ufike Mbali. #Moto🔥Bonyeza Link kwenye Bio☝🏾️apo Juu Kusikiliza,” aliandika Nay wa Mitego Insta
Hata hivyo mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii wamedai alichokifanya Young Killer Msodoki ni kitu sahihi kutokana na rapa huyo kuzoea kuwachana wasanii wenzake.
Kupitia wimbo ‘Moto’ ya rapa huyo alimchana Young Killer kwamba ameshindwa muziki na anatakiwa kurudi nyumbani kwao Mwanza

Comments

Most Viewed in KevNationmedia

Mapenzi: style za kufanya mapenzi na mwanamke/msichana mjamzito

Newz: Je? unayajua madhara ya kutofanya tendo la ndoa kwa mda mrefu?